December 11, 2020

 


UONGOZI wa Yanga, umerudi tena Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiandika barua kuomba majibu ya ukiukwaji wa usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Morrison kwenye mfumo wa TMS.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu kiungo wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya aliyesajiliwa na timu hiyo usajili wake kuonekana na matatizo kabla ya kufungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) sambamba na kutozwa faini ya dola 130,000 (Sh 300Mil).


Kichuya alijiunga na Simba, Januari, mwaka huu akitokea Pharco ya Misri huku taarifa zikisema aliondoka bila ruhusa. Kwa sasa anaitumikia Namungo FC.

 

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Yanga ambayo Spoti Xtra imeiona, imeandikwa Desemba 4, mwaka huu kwenda TFF kuomba majibu ya barua yao waliyoiandika Septemba 28, 2020 juu ya ukiukwaji wa usajili wa Morrison.

 

Barua hiyo imeandikwa baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF kuamuru Morrison kuwa huru baada ya kubainika mkataba wake na Yanga kuonekana una upungufu.


Baada ya mkataba huo kuonekana na upungufu, kamati hiyo ilimruhusu Morrison kujiunga na Simba msimu huu, akisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Barua hiyo iliyoandikwa na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, ilieleza Yanga imejiridhisha bila shaka Morrison alisajiliwa na Simba kwa makosa yaleyale au zaidi, hivyo kuiomba kamati kufanya maamuzi kama waliyoyafanya kwa Yanga.

 

Aidha, barua hiyo ilieleza kuwa Yanga wanataka kupata ufafanuzi na maamuzi yafanyike kwa Klabu ya Simba kama yalivyofanyika kwao, hiyo ni baada ya kupita muda mrefu bila ya kutolewa majibu hivyo, klabu hiyo inaomba kupatiwa taarifa ya maendeleo ya suala hilo na majibu stahiki kabla ya usajili wa dirisha dogo kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

 

Yanga imeonekana kushtukia jina la kiungo huyo kuingizwa kwenye mfumo wa TMS katika dirisha dogo la usajili baada ya kupata taarifa za jina la Mghana huyo kutokuwepo katika mfumo baada ya usajili mkubwa kushindikana kuliingiza jina lake.

 

Endapo itabainika kuna mapungufu hayo, huenda Morrison naye akafungiwa kama ilivyo kwa Kichuya aliyefungiwa kutocheza soka kwa kipindi cha miezi sita.

11 COMMENTS:

  1. Mambo mengine yanachosha, hilo suala linasaidia nini mpira wa tanzania? Watu wanakufa na bado waliobaki maisha yanaendelea, itakuwa mtu kahama timu? Huyu ni wa kwanza? Kama wanamtaka sana wakamchukue basi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga mchecheto wanauhofu mziki wa simba sasa wanajaribu kucheza na matukio.Kuna ushahidi yakwamba yanga walifoji saini kwenye moja ya mkataba wa Morrison kitu ambacho TFF waliamua kutumia busara kumaliza suala hilo kishkaji la sivyo Yanga ingekuwa ipo pabaya hivi sasa ila mwana kulitafuta mwnana kulipata.

      Delete
    2. Habari zack kufoji ni uzushi.kosa waliloadhibiwa ni kufuta sehemu fulani Ktk mkataba na walitoa sababu kua walikopi mkataba wa zamani ktk tms,na kufuta yasiyohusika,maana ukitunga wako.haukubaliki lazima uwe uleule wa kwenye tms.na hoja nzito zaidi ni kwamba mapungufu ya mkataba hayavunji mkataba ila manne.kulazimishwa,kutokuwepo thamani ya pesa kua under18,na kukosa akili timamu.

      Delete
  2. Swala la Mwakalebela kusema wanamsajili chama wakati yupo ndani ya mkataba limeishia wapi au walivyomrubuni Senzo

    ReplyDelete
  3. Yaani hayupo kwenye mfumo wa TMS huku anacheza?Huu ujinga Yanga wataacha lini?Timu yangu Yanga tufuate ushauri wa Rais mstaafu Kikwete. Wachezaji huwa wanahama.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe sio yanga jiulize kichuya kwenye tms anaomekana yupo timu gani?na simba wanaadhibiwa kwanini?hii ni vita ya kuondoa ubabaishaji sio kudai mchezaji.

      Delete
  4. Hawahami wakiwa ndani ya mkataba...linakuja hilo. Itakuwa mwisho wa uswahili uchwara.

    ReplyDelete
  5. Mkataba ambao TFF walisema haupo kisheria au kuna mwingine?
    FIFA wana mkataba mwingine au ndio huo huo uliochanwa na kukataliwa na TFF??

    ReplyDelete
  6. Simba ni mapunga tuu

    ReplyDelete
  7. Eymael anawajua nyani kazi yao kubweka kama mbwa.Mfano huu hakukosea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic