December 27, 2020


 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’, ameahidi kutumia zaidi ya Sh milioni 500 ili amshushe straika mpachika mabao atakayeingia moja kwa moja kikosi cha kwanza ambapo ametajwa kuwa ni staa wa Orlando Pirates, Jean Makusu, na imeelezwa kuwa wapo kwenye hatua nzuri.

 

Pamoja na Makusu kuwa kwenye mkataba na timu ya RS Berkane ya nchini Morocco akiwa anaichezea Orlando kwa mkopo, bado Mo amevutiwa naye japo dau lake likitajwa kufi kia Sh milioni 800, ambazo Mo amekubali kutoa nusu au robo tatu ya kiasi hicho cha fedha.


Mkataba wa Makusu unatarajiwa kufikia ukingoni Juni, mwakani, hii ni kwa taarifa ya umiliki wake ambayo ni Kampuni ya Bro Management ambayo ina wamiliki pia wachezaji wengine wa Ligi Kuu Bara, Mukoko Tonombe wa Yanga na Clatous Chama wa Simba.

 

Chanzo kimeeleza kuwa Simba ilikuwa kwenye mazungumzo na kiungo wa Plateau United ya Nigeria, Oche Ochewechi, ila wamebadili kwanza baada ya kuona mahitaji makubwa upande wa safu ya ufungaji kuelekea kwenye michuano ya kimataifa ambayo lengo lao la kwanza ni kufika hatua ya nusu fainali.


Kwenye dirisha hili dogo, sisi malengo yetu yalikuwa ni kuongeza beki na kiungo mkabaji na hili lilikuja baada ya kumsajili Chris Mugalu, ila kadiri muda unavyosonga mbele tunaona mahitaji ya ufungaji nayo yanakuwa makubwa na hili ameliona zaidi mwenyekiti wetu wa bodi, Mo.


Kufuatia hali hiyo sasa amelazimika kufuatilia uwezo wa kushushiwa gharama ya Makusu ili tuone kama ataweza kuendana na gharama inayotajwa kisha tuingie mezani na wamiliki wake kwani tayari tulishafanya mazungumzo ya kina na nyota mwingine wa Plateau United ambaye tumesimama kidogo ili tuone uwezekano wa kumpata Makusu,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo:Championi

6 COMMENTS:

  1. We mwandishi ni mavi maana unasema et makusu yuko Orlando arafu hapo hapo una unasema anamkataba na Fc Berkane ya morroco! We zwazwa tu

    ReplyDelete
  2. Ninavyoijua simba hakuna muandishi wa habari anaejua mipngango yao ya usajili hizo zitakuwa ni tetesi tu.Ila tuwe serious na wakweli kabisa na kama Mo atasikia basi na asikie.kama Barbara atasikia basi asikie.kama magori atasikia basi na asikie,kama mashabiki wa simba watasikia basi na wasikie pia na waache kumsakama kocha wao.Mbeligiji yule hana hofu yeyote ya maisha au ya kupoteza ajira. Sven yupo serious na kazi na hana anachokiwaza isipokuwa kuitumikia simba hapa Tanzania,yupo professional zaidi. Mapungufu binaadamu yeyote hakosi.Wanayanga wanamchukia sana Sven na watafurahi sana akiondoka simba.Yanga wanamcheka kagere kuwa mzee lakini wanafurahia tetesi za kagere kusajiliwa na Yanga? Kwa hivyo mashabiki wa simba kwa kiasi fulani wametekwa akili na mashabiki wa yanga kuisema vibaya timu yao ya simba inashangaza sana.Ila simba kama watazembea kufanya usajili wa maana kwenye dirisha dogo basi Yanga bingwa na hahihalisi kama kocha simba atafukuzwa au la kwani tatizo la simba sio kocha ni la wachezaji wa simba kucheza mpira kwa mazoea wakati timu nyingi kwenye ligi zikionekana kukamia mno labda kuna ahadi kutoka upande fulani kugharamia zawadi za wachezaji wa timu fulani kama wataifunga timu fulani.ushindani wa maana kwenye ligi sio kitu kibaya ni jambo zuri kwa afya ya makuzi ya soka letu Tanzania.kwa maneno mengine unaweza kusema wachezaji wa simba wanaonekana kushindwa kudiliva kilichotarajiwa na wengi yaani kushindwa kucheza kwa ubora uliotarajiwa. Usajili wa simba ulionekana mkubwa na wa wachezaji wakubwa lakini usajili wa Mukoko na tusila kisinda Yanga ni mkubwa zaidi kabla hata hajaja saido. Usajili wa Never tegere,prince dube na monzizi kwa Azam ni mkubwa pia na ili simba kubakia kwenye gemu yao lazima wanahitaji wachezaji wawili au watatu wakubwa kiviwango kuja kuleta laza tofauti kwani kikosi cha simba karibu miaka mitatu ni kile kile sasa wachezaji wao wengi hasa wale tegemezi mbinu zao zinajulikana tayari ni rahisi mno kukabwa na kushindwa kuwa msaada kwa timu uwanjani.Kocha atalaumiwa,atafukuzwa lakini bila marekebisho ya kikosi kazi bure.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Andiko refu lakini pumba! Yanga haiwezi mchukia kocha wa Simba na hasa wakati huu ambapo wanafanya vizuri kileleni. Ingekuwa kuzoea kunakufanya ukabwe kiurahisi basi Mess asingekuwa anacheza kabisa.

      Delete
    2. Andiko la huyu mkuu ni kubwa kuliko uwezo wako wa uelewa. Otherwise wala usingepingana naye. Anyway msimu huu wa sikukuu bangi zinauzwa kwa bei ya promoshen

      Delete
  3. Ivi Yanga imchukie sven kwa lip mbona mnateseka

    ReplyDelete
  4. Andika tu ili uuze ila ukweli hakuna club inaweza mleta Makusu bongo. Kama ilishindikana bwalya kumtoa Zambia, mtaweza kumtoa Makusu SA tena akiwa kwenye kiwango bora!? Kwanza ana Mwezi tu toka atue SA na katika mechi mbili alizocheza ametupia na kutoa assist. Endeleeni kucheza mpira wa media tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic