December 18, 2020

 


LEO Desemba 18 kikosi cha Simba kinatarajiwa kukwea pipa kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.


Wachezaji watatu wanatarajiwa kubaki ndani ya ardhi ya Bongo wakiendelea kufanya program ambazo wataachiwa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck. 


Wachezaji hao ni pamoja na Charles Ilanfya ambaye ni mshambuliaji namba nne wa Simba,Larry Bwalya ambaye ana matatizo ya kifamilia na Thadde Lwagga ingizo jipya ndani ya kikosi.


Simba itacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Januari 6, Uwanja wa Mkapa.

Ikiwa itashinda kwenye mchezo wa kwanza na kuweza kulinda ushindi wake kwenye mchezo wa marudio utakaochezwa Bongo, Simba inaweza kutinga hatua ya makundi.

2 COMMENTS:

  1. Simba Kuna tatizo Ila hawasemi na tatizo ilo litafanya washindwe kuchukua kombe la ligi pia litawafanya wasifike mbali klabu bingwa lali bwalya matatzo yake hayaishi ya kifamilia kila siku na pia huyo lwanga si alisajiliwa ili kucheza klabu bingwa Sasa kwanini hakujumuishwa au kocha hajui anachoitaji tuna sajili wachezaji wake kukaa benchi au kwa miemko hacheni usaniii Simba na viongozi hata sakata la kichuya Kuna viongozi wa Simba wamekula hela

    ReplyDelete
  2. Ukishapata list rasmi ya wachezaji waliyoondoka, rudia tena comment yako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic