NYOTA wa Yanga, ingizo jipya Saido Ntibanzokiza kesho anatarajiwa kuanza kuonyesha makeke yake ndani ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 37 watakuwa wenyeji baada ya kuomba iwe hivyo.
Nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru tayari vibali vyake vya kazi vimekamilika kilichobaki ni kocha kuamua kama anahitaji huduma yake au lah.
Tayari akiwa Bongo amecheza mchezo mmoja wa kirafiki ilikuwa dhidi ya Singida United ambapo alifunga mabao mawili wakati Yanga ikishinda 3-0 Uwanja wa Liti ambao zamani ulikuwa unaitwa Namfua.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa tayari utaratibu wa vibali kwa Ntibanzokiza umekamilika kwa kufuata utaratibu hivyo anaweza kuanza kutumika ndani ya kikosi.
"Tayari kila kitu kuhusu mchezaji wetu Ntibanzokiza kimekamilika kwa kuwa tumepata leseni hivyo anaweza kuanza kucheza ndani ya ligi," .
0 COMMENTS:
Post a Comment