December 5, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroek amesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Plateua United utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao wanahasira ya kulipa kisasi kwa kuwa walifungwa wakiwa nyumbani.


Simba itawakaribisha wageni wao Plateau United ambao jana Desemba 4 waliwasili Dar na kupokelewa na mashabiki waliopo Tanzania ambao walikuwa wamevaa jezi za njano na kijani huku wakiongea kiswahili safi kabisa.


Mchezo wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0 leo ina kazi ya kulinda ushindi wao na kuongeza mabao mengine ili kusonga mbele hatua ya mtoano.


Sven amesema:"Utakuwa mchezo mgumu na tutapambana ili kupata matokeo, tunaamini kwamba wapinzani wetu wameshatambua aina yetu ya uchezaji ila haitupi hofu.


"Kila kitu kipo sawa mchezo wetu wa kwanza umepita na sasa tuna kazi nyingine ya kusaka ushindi kwenye mchezo ambao tutakuwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti," .

3 COMMENTS:

  1. Simba itawakaribisha wageni wao Plateau United ambao jana Desemba 4 waliwasili Dar na kupokelewa na mashabiki waliopo Tanzania ambao walikuwa wamevaa jezi za njano na kijani huku wakiongea kiswahili safi kabisa.

    ..........................

    Nimeipenda hii..weww kweli.mwandishi, hujataka kusema ni mashabiki wa Yanga eeh

    ReplyDelete
  2. Ha ha ha. Hapo umeua, ni mashabuki uchwara wa yanga

    ReplyDelete
  3. Aka kamwandishi niwa itulopolo ila sio dhambi jamani nae ana moyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic