December 5, 2020

 


MSHAMBULIAJI Stephen Sey nyota wa Namungo raia wa Ghana anatajwa kuingia rada za Yanga ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kwa lengo la kuboresha safu ya ushambuliaji.


Ikiwa ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 imefunga jumla ya mabao 15 na mtupiaji wao namba moja ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu.

Namungo ikiwa inashiriki michuano ya kimataifa Sey amekuwa mhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho kwa kuwa kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex wakati ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Al Rabita alitupia mabao mawili.

Kasi yake ambayo imekuwa na mwendelezo baada ya kuwafunga Yanga kwenye ligi walipokutana inatajwa kuwa sababu ya kuwavutia mabosi wa Yanga ambao wapo kwenye mchakato wa kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebea amesema kuwa kwa sasa wanasubiri ripoti ya mwalimu Kaze ili kujua kama anahitaji kufanya usajili mwingine ama la.

9 COMMENTS:

  1. Ni kweli tuna uhaba wa washambuliaj ongezeni nguvu ubingwa wetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hamna uhaba ila mna washambuliaji wabovu ambao Kaze alijinasibu kuwa na wazur na alihusika kwenye usajili wao

      Delete
  2. Sey anaweza kuwa ni suluhisho la uhaba wa mabao mengi Jangwani akishirikiana na Saido

    ReplyDelete
  3. Nchimbi na Tarick waliwafunga hatrick mkawachukua na huyu amewafunga mnataka Kumchukua , hadi msimu ukamilike tutasikia mengi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usijisahaulishe kwamba Adam Salamba, Ilamfya na Mohamed Rashid waliwafungeni pia, mkawachukua. Waliko sasa nakuachia homework. Kabla ya kusema geuka pande zote

      Delete
    2. Ameongea tu kiushabiki bila kuangalia wao wameharibu viwango vya wachezaji wangapi waliowasajili baada ta kuwafunga. Halaf kipind hiki mikia wana hasira hasira sana hata kwenye mambo ya kawaida kama wanawake wajawazito. Au mimi peke yangu nawaona wako hivyo?

      Delete
  4. Kusikia ni faradhi kwa kila mwenye masikio yaliyohai

    ReplyDelete
  5. Yaani kuwafunga Sudan kusin Na Yanga ndio mmeona Bonge la mchezaji Hana tofauti Na Yipe

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic