December 12, 2020


 DAKIKA 90 leo Uwanja wa Mo Arena zimekamilika kwa timu ya Simba Queens kugawana pointi mojamoja na Yanga Princess kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake uliokuwa na ushindani mkubwa.


Hii inakuwa ni dabi ya kwanza kwa Yanga Princess kusepa na pointi moja kwa kuwa kwenye mechi nne za misimu miwili iliyopita walikwama kusepa na pointi tatu mbele ya Simba Queens.

Chini ya Mussa Mgosi ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba leo ameshuhudia vijana wake wakimaliza dakika 90 bila kuambulia bao wakiwa nyumbani.


Edna Lema naye pia ameshuhudia vijana wake wakimaliza dakika 90 bila kushinda leo kwa mara ya kwanza kwa msimu wa 2020/21 kwa kuwa kwenye mechi tatu za mwanzo zote walishinda na kusepa na pointi tisa.


Licha ya sare ya bila kufungana, Yanga Princes inabaki kileleni ikiwa na pointi 10 kwa kuwa imeshinda mechi tatu na sare moja.


Simba inafikisha pointi nane kwa kuwa imelazimisha sare mbili na kushinda mechi mbili kwa msimu wa 2020/21 ikiwa na kazi ya kutetea taji la Ligi ya Wanawake.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic