December 28, 2020


 IMEELEZWA kuwa nyota wa kikosi cha Simba, Clatous Chama kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na mabosi wa timu hiyo wakimshawishi aongeze mkataba mpya ndani ya kikosi hicho.

Habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa wamefikia hatua nzuri ya mazungumzo jambo linalotoa matumaini kwa Chama kusaini mkataba mpya.

"Kwa sasa bado Chama hajasaini mkataba na amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi ili aweze kusaini kwani ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi.

"Imekuwa akitajwa kuwa kwenye mazungumzo na Yanga jambo linalowapa presha viongozi hasa ukizingatia ni mchezaji muhimu kikosi cha kwanza," ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni uongozi wa Simba uliweka wazi kwamba umemalizana na nyota huyo ambapo atabaki ndani ya kikosi hicho mpaka 2023 jambo ambalo linatajwa kuwa bado halijakamilika.

Mkataba wa Chama ndani ya Simba kwa sasa umebakiza miezi sita na anaruhusiwa kuzungumza na timu ambayo inahitaji huduma yake kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

Ndani ya Simba kwa msimu wa 2020/21 amehusika kwenye mabao 12 kati ya 33 ambapo amefunga mabao sita na kutoa pasi sita za mabao.


11 COMMENTS:

  1. Huu sasa utoto, si tuliambiwa chama kalamba 800m?

    ReplyDelete
  2. MO awafanya Mikia MBUMBUMBU kwa mara nyingine tena!

    ReplyDelete
  3. Hawa wandishi wa habar wanakosa habari za kuandikwa ndo maan wanahangaika kumuongezea chama ili habar zao zisomwe na wao waweze kufaidika

    ReplyDelete
  4. Hahahahahaahha jaman nacheka kww dharau jamn,, mo mo mo ulisema chama amesain mkataba Hadi 2023 leo hata miezi miwil unasema mpo kwenye mazungumzo

    ReplyDelete
  5. Hahahahahaahha jaman nacheka kww dharau jamn,, mo mo mo ulisema chama amesain mkataba Hadi 2023 leo hata miezi miwil unasema mpo kwenye mazungumzo

    ReplyDelete
  6. Ukisikia nguruwe fc usishangae, yan mo anawafanya mazuzu na mwisho wa siku CHAMA huyooooo make waliambiwa kaongezewa mkataba kumbe walaa

    ReplyDelete
  7. Huu ni utoto sasa si mlisema na mkaandika chama kapewa milioni 700 kwa miaka 2 leo tena mzungu yameanza? Si ushoga huwo sasa? Jana nasoma tena wameandika kagere kasaini yanga miaka 2 ujinga na upumbavu wa kudanganyana

    ReplyDelete
  8. Kagere kuja yanga haiwezekan uwa anajifanya simba ndo kafika

    ReplyDelete
  9. Sasa mbona yanakuwa yanaandika uongo tu? Huuu upumbu sana kwakwel nachukia sana magazeti dah

    ReplyDelete
  10. Mo alimsainisha mwezi mmoja CHAMA YUKO KWENYE MWAKA WAKE WA MWISHO WA MKATABA HAKUNA MTU ANAMFORCE KUSAINI NI YEYE MAISHA YAKE YA SOKA NA FAMILY YAKE ANA CHOICE saying that na hivi ni mwafrica ataangalia wapi kuna maslai sio mapenzi na future ya kucheza sio kukaa benchi sasa huyo muongo wenu kama kocha wenu alivyo muongo na kadu nae muongo na hao wapambe nao waongo kama Rage basi mnawadanganya hao mbumbuu wenu kumbe uwezi kulazimisha mtu kama anataka kuona mkataba wake unakuwa wzi ili awe free agent alambe mpunga mwingi au hamjui hilo. chama hana mkataba na simba zaidi ya huu unaokwisha hiyo ndio fact mbumbuu fc aka mikia buanaaa -:))))))

    ReplyDelete
  11. Mo alimsainisha mkataba hewa? Au alikua anatudanganya propaganda zake kugeuza uhalisia, lkn Kwann adanganye itasaidia nn?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic