December 23, 2020


WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo wameanza kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya FC Platinum kwenye mchezo wa hatua ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe.

Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kilishuhudia bao la kwanza likifungwa na Perfect Chikwende dakika ya 17 baada ya mabeki kufanya makosa ya kumuacha nyota huyo awapite.


Licha ya jitihada walizofanya Simba kuweka usawa mzani bao hilo kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa kuwa hawakufanikiwa.


Bao la Chris Mugalu dakika ya 78 lilitaka kuwarudisha kwenye reli ila mwamuzi alikataa kwa kueleza kuwa mfungaji alikuwa ameotea.

Kupoteza mchezo wa kwanza, Simba ina deni la mabao zaidi ya mawili Uwanja wa Mkapa Januari 5.


Kipa Aishi Manula hakuwa na chaguo la kufanya na kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwa mara ya kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Mechi mbili mbele ya Plateau United aliweka lango lake salama kwa kukaa bila kufungwa ila leo amekwama.


FC Platinum wameonekana kuwa na spidi na mbinu ndani ya uwanja jambo lililowapa kazi Simba kupata ushindi.

19 COMMENTS:

  1. Hawatoki kwa Mkapa lazma wafe tu hao platnum

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekalili tu mpira, kwa Nini wasitoke?

      Delete
    2. Sven kazihirisha ubora wake kimataifa bonge la kocha ila tatizo lipo kwenye wachezaji wenyewe. Vipi utamlaumu Sven kwa goli walilofungwa simba na platinum? Mbinu alizoingia nazo Sven kama angekuwa na wachezaji makini hivi sasa tunazungumza mambo mengine.Ndani ya kikosi cha simba kuna matatizo ya muda mrefu na bado yanaendelea kuigharimu timu.Nafasi ya mshambuliaji mwenye vurugu na uthubutu wa kucheza na mabeki wa timu pinzani.Mfano mzuri ni lile goli walofunga platinum ni kwa jitihada na uthubutu wa mchezaji binafsi.Boko na kagere umri umekwenda kufanya vurugu za aina ile. Wawa ameshasababisha magoli ya aina ile mara nyingi. Kwa nini wawa beki mzoefu anashindwa kujipanga beki mmoja akimtangulia mwenzake mbele mmoja lazima abaki nyuma. Viungo wakabaji na wachezeshaji wa viwango wenye roho mbaya. Tunaona amekuja Lwanga kutoka Uganda ngoja tuone anini ila anaonekana yupo vizuri.Viongozi wasichelewe kuongeza kiungo mchezeshaji wa ziada na ikiwezekana beki pia. Viongozi wanatakiwa kuacha uoga na kuondosha mughali huku timu ikiendelea kuwakatisha watu tamaa.Kama ulimsikiliza Sven vizuri baada ya mechi ya platinum basi utaona analia kwa kukosa wachezaji ambao wanauwezo wa kwenda kutimiza majukumu yao uwanjani ipasavyo.mchezaji.Na Sven akaenda mbali zaidi kwa kusema hata Boko angekuwa yupo uwanjani hafikirii kma kingebadilika kitu kwenye ile mechi. Maana ake nini? Kocha anademand kussjili baadhi ya nafasi za wachezaji wenye uwezo zaidi kimataifa pengine hata ligi ya ndani.Simba tayari inamsingi mzuri ya wachezaji waandamizi ila haijakamika kiasi kwamba utaona hata Sven hana kikosi cha kwanza. Wachezaji wapo ila sijui hawakitambui au nini? Tizama muzamiru mechi kama nne bado anaendelea kufanya makosa yale yale ya kukosa umkini na kupoteza mipiza hovyo.

      Delete
    3. We unaye mwambia huyo kakariri na wewe vile vile umekariri unaleta ubishi wa kubishana na Redio akili zenu zilivyokuwa fupi mnadanganywa na wachambuzi feki eti yasije yakatoke aya UD SONGO, yani wale Platinum kama kwao wamecheza vile basi tunawaambia UTOPOLO kawapokeeni vizuri nunueni jezi zao lakini kitakachowakuta hao Platinum wataenda kuadisia kwao Zimbabwe hizo ndo mechi za watu kama wakina Chama. Ndegeresi

      Delete
  2. Kumbe Mugalu akifunga goli likakataliwa???

    ReplyDelete
  3. Simba hakuna kocha pale,tusidanganyane wadau.Kocha uwezo wa mpira ni mdogo mno.

    ReplyDelete
  4. Kwenye kocha ni wapi

    ReplyDelete
  5. Asante sana fc PLATINUM, kelele za nguruwe huku kimyaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan hujui Kama Kuna dk 90 nyingine, kweli utopolo hawajielewi

      Delete
    2. We churaaaa, Utopolo, Kandambili, Yebo Yebo hii ni ngoma ya wanaume, wewe endelea kukuna nazi na IHEFU FC huku ukijiongopea kuwa una timu ya mpira kwa kuwafunga timu ambayo hata mshahara wao hawajui wanapataje kama unafikiri Simba kufungwa ilo goli moja mmetunyamazisha basi wewe utakuwa sio mzima, Nkana walishinda 2-1 mkaja kwa wingi kuwashangilia mbaasha zenu kutoka Zambia lakini mliondoka na aibu sasa tunwaambia sisi ndio simba hmkawii kusema tumeuloga uwanja wa taifa tukutane kwa mkapa Jan 5 inshaalah

      Delete
    3. Hawakawii kuropoka tumeweka madawa kwenye vyumba vya wachezaji

      Delete
  6. Platinum kama ndo inacheza vile basi wasubiri mvua kwa mkapa

    ReplyDelete
  7. Kocha hakuna pale hii ndio mechi ya mwisho kwetu tukubali tukatae mm mwanachama ukweli ndio huo

    ReplyDelete
    Replies
    1. We utakuwa Tahira we unataka kocha afanye nini zaidi ya alichokifanya, Simba ndo imetengeneza nafasi nyingi

      Delete
  8. Platinum walikuwa wanaweweseka wanajua safari imefikia mwisho. Kocha wao alikataa kuongea na waandishi wa habari.
    Kwa Mkapa ndio mwisho wa stori.

    ReplyDelete
  9. Wewe Utopolo weka namba ya uanachama tuione. Utopolo hii vita ya wakubwa. Vita ya wavulana itachezwa baadaye.Kawapokeeni na hawa pia.

    ReplyDelete
  10. Acheni kumlalamikia kocha Hana shida wachezaji wetu hawajitambui

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic