December 27, 2020


KLABU ya soka ya Simba kwenye mchezo wa kombe la FA imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya  Majimaji ya Songea.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji ambaye leo amekuwa mbongo licha ya timu yake kushinda ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza na kupata ushindi.

Bao la kwanza lilifungwa na beki wa Simba Gadiel Michael dakika ya 3 baada ya Said Ndemla kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kukutana na Gadiel ambaye alikuwa nahodha kwenye mchezo wa leo.

Mshambuliaji aliyeanza kikosi cha kwanza leo Chris Mugalu alipachika bao la pili dakika ya 16 na liliwafanya waende kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wameshinda mabao mawili.

Kipindi cha pili beki wa kati Ibrahim Ame alipachika bao la tatu dakika ya 78 na mshambuliaji namba moja wa Simba, Meddie Kagere alipachika bao dakika ya 78.

 Wakati Majimaji ambao walikuwa wakifanya mashambulizi kwa kumtumia Ismail Mussa wakiamini kwamba mchezo umekamilika Luis Miquissone alifunga bao la tano dakika ya 88.

Ushindi huo unaifanya Simba kutinga hatua ya nne baada ya kuiondoa Majimaji leo ambayo inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.


Sven amesema:"Sitaki kuskia wachezaji wangu wakikosolewa kwa kuwa wanafanya kazi kubwa kweli,".

8 COMMENTS:

  1. bomu limeenda kulipukia mochwari 😂😂😂

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na waliyopita bure limeripukia makaburini!

      Delete
    2. True, wamepotea bure Kama vilema vile

      Delete
  2. Wandugu ivi ni kwa nini mechi za Yanga, simba, Namungo, mtibwa kwenye kombe la FA hz timu ni wenyeji hawapangiwi kuzifata hiz timu ndogo Kuna nini kilichojificha.

    ReplyDelete
  3. Bado kidogo Utopolo mtaanza kusingizia conspiracy.Mzee wa conspiracies naona bado upo.Huwa mnaongoza wanaume wakija ohh kabebwa,ohh marefa ohh TFF.

    ReplyDelete
    Replies
    1. bomu limelipukia mochwari mpigaji anajitokeza hadharani akijigamba kuua! 😂😂😂😂

      Delete
    2. Ni lipi bora bomu kulipukia mochwari au kupangiwa timu hewa ili uhesabiwe umefuzu hatua inayofuata?

      Delete
    3. Utopolo hawana akili wanafurahia kupita bure yaani kula chakula ambacho hawajakifanyia kazi Wala kukitolea jasho. "Wanapenda vya bure IPO siku wataliwa wataanza kutoa povu"

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic