December 8, 2020


 IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga wapo kwenye mpango wa kuipata saini ya beki wa zamani wa Klabu ya Nkana FC ya Zambia, Hassan Kessy ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Mtibwa Sugar.


Kessy ambaye amesaini dili la miaka miwili ndani ya Mtibwa Sugar kwenye usajili wa dirisha kubwa kabla ya kutua ndani ya kikosi hicho kilichokuwa chini ya Zuber Katwila alihusishwa kujiunga na Yanga kabla dili lake halijabuma.

Kwa sasa Mtibwa Sugar inanolewa na kocha msaidizi Vincent Barnaba huku Katwila akiwa zake ndani ya Ihefu FC.

Habari zinaeleza kuwa Yanga inataka kuimarisha zaidi kwenye safu ya ulinzi hasa baada ya mshambuliaji wao Michael Sarpong kuanza kupata muunganiko na wachezaji wengine akiwa amefunga mabao manne.


"Kessy alikuwa kwenye mpango wa Yanga hata kabla hajarejea ndani ya Mtibwa Sugar ila kuna mambo hayakwenda sawa jambo lililopelekea akaibukia huko aliko.


"Hata dili lake la Nkana aliachana nalo kwa kuwa alikuwa amepewa ofa ndani ya Yanga hivyo bado kuna mpango ambao upo wa kumrejesha kikosini mambo yakiwa sawa atarejea," ilieleza taarifa hiyo.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejipanga kufanya vizuri kwenye ligi hivyo watashusha majembe ya kazi.

5 COMMENTS:

  1. Kessy huyu?Hana hadhi ya kurudi hapo,Ana papara Na rafu za kijinga.

    ReplyDelete
  2. Mnasema beki WA Zambia kwahiyo Yanga wakimchukua wanalipa hela ya uhamisho Nkana au Mtibwa?Inaonekana Enzi ukisoma hukuwahi kupata swali la kutafuta kichwa cha habari.

    ReplyDelete
  3. Hutu atakuwa hajielewi, amesahau yaliyompata kipindi kile?

    ReplyDelete
  4. Huwa unalipwa kufanya Promo kwa wachezaji? Huyu Kessy aliyeisha kabisa ndio acheze Yanga? Mtafutie kwingine Yanga unajidanganya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic