December 8, 2020

 


KWENYE Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi zote mbili Shomari Kapombe dhidi ya Plateau United aliyeyusha dakika 90.


Hivyo ametumia jumla ya dakika 180 kimataifa msimu wa 2020/21. 


Beki huyo mzawa amekuwa na kiwango bora ndani ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck. 


Vandenbroeck amesema kuwa anafurahishwa na uwezo mkubwa wa wachezaji wake wote ambao wameonyesha ndani ya Uwanja anaamini watafikia mafanikio ambayo wamejiwekea kitaifa na kimataifa.

"Kila mchezaji anapambana ndani ya Uwanja kuonyesha kile ambacho anacho hilo ni jambo zuri na la muhimu kwa kila mchezaji kulitambua.

"Tuna kazi kubwa ya kufanya ndani ya ligi kuu kutetea  ubingwa na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika bado kazi haijaisha hivyo tutaendelea kupambana," amesema. 


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic