December 23, 2020


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kwamba unawaombea dua watani zao wa jadi Simba waweze kufanya vizuri kwenye mechi zao za kimataifa ikiwa ni pamoja na mchezo wa leo dhidi ya FC Platinum.

Simba ina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya FC Platinum baada ya kupenya hatua ya awali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau FC ya Nigeria.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wanatambua kwamba wapinzani wao wapo nje kwenye mashindano ya kimataifa ila dua yao ni kuona wanafanya vizuri.

“Sisi huku tunaendelea kupambana kwenye ligi na mechi zetu hivyo nao pia tunawaombea dua wafanye vizuri, lakini wasisahau kwamba nasi pia tunafanya vizuri na watuombee” alisema.


Yanga leo ambayo imeanza kumtumia nyota wake mpya Saido Ntibanzokiza akiwa ametumia jumla ya dakika 125 uwanjani kwenye mechi mbili.


Moja ilikuwa ya kirafiki dhidi ya Singida United ambapo alitumia dakika 80 na wa pili ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji, alitumia dakika 45 akiwa amefunga jumla ya mabao matatu, mawili kwenye mchezo wa kirafiki na moja kwenye ligi.


Leo ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Chanzo:Championi 

2 COMMENTS:

  1. Mnajua wakitolewa watawekeza nguvu nyingi kwenye ligi ya ndani

    ReplyDelete
  2. Hakuna duwa zaidi ya fitina wanajiosha tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic