KOCHA Mkuu wa Klabu ya Al Hilal ya Sudan, Zoran Manojlovic amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
Al Hilal ni miongoni mwa timu tatu ambazo zinashiriki mashindano ya Simba Super Cup huku waandaaji wakiwa ni washiriki pia ambao ni Simba.
Mchezo wa kwanza wa ufunguzi, Uwanja wa Mkapa, Januari 27 ilikubali kupoteza kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa walikuwa wamechoka kutokana na safari ndefu ya kutoka Sudan.
Leo inakuwa ni mchezo wake wa pili na wa kwanza kwa TP Mazembe ya Congo ambayo anacheza pia Mtanzania Thomas Ulimwengu.
Zoran amesema:"Kikubwa ni kwamba wachezaji wangu kwa sasa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe na tuna amini kwamba tutapambana kusaka ushindi.
"Kupoteza mchezo wa kwanza haina maana kwamba tumepoteza kila kitu bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi yetu dhidi ya TP Mazembe,' .
AL HILAL timu chovu bora hata ingekuwa Mashujaa mtu angeenda kupoteza muda kwenye screen
ReplyDeleteHuyo ana mana kuwa Mnyama alipata timu chofu ndio wakaweza kuifungwa 4G
ReplyDeleteMnyama kaonesha umahiri na ubingwa wake anaestahaki kuutetea tena na kuonesha wazi kuichapa timu shupavu Al Hilal nne moja na baadae hiyo Al Hilal muweza kuu hapa TP Mazembe timu ambayo imewahi kuchukua ubingwa wa klabu bingwa Africa. Iliyobaki upige hesabu zako mwenye we vipi mambo yatakuwa pale Mnyama atapokabiliana na Mazembe. Kweli Mnyama atanguruma
ReplyDelete