BAADA ya kupewa mapumziko mafupi leo Januari 25 kikosi cha Azam FC kinatarajiwa kurejea kambini.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakari Thabit amesema kuwa mapumziko ambayo walipewa wachezaji yalikuwa ni ya siku mbili.
Kambi ya Mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Mapinduzi wakiwa na mataji matano ilikuwa Zanzibar ambapo huko walicheza michezo mitatu ya kirafiki.
Kwenye hiyo michezo mitatu walipoteza mmoja na kushinda miwili hivyo wanarejea tena kuendelea pale ambapo wakiishia.
"Wachezaji walipewa mapumziko mafupi na Jumatatu,(leo) wanatarajiwa Kurejea kambini ili kuendelea na maandalizi kwa ajili ya Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine," .
0 COMMENTS:
Post a Comment