January 19, 2021



BAADA ya mabosi wa Simba kukamilisha usajili wa nyota wa Klabu ya FC Platinum, Perfect Chikwende sasa inatajwa kuwa nyota wengine watano wapo kwenye rada za kutua ndani ya kikosi hicho.

Nyota anayetajwa kumalizana na Simba ambayo kwa sasa ipo chini ya Kaimu Kocha Seleman Matola ni kiungo wa DC Motema Pembe, Karim Kiekie.

Nyota huyo anakipiga pia kwenye timu ya Taifa ya Congo na yupo na timu ya Taifa ya Congo ambayo inashiriki michuano ya Chan.

Anatajwa kuwa miongoni mwa vijana wanaofanya vema ndani ya uwanja kwa uwezo wake wa kutumia mguu wa kushoto.

Mwingine anayetajwa kuwekwa kwenye rada za Simba ni pamoja na Peter Mudawa raia wa Zimbabwe ambaye anacheza ndani ya Klabu ya Highlanders.

Na mshambuliaji raia wa Nigeria Junior Lukosa naye anatajwa kumalizana na mabosi hao kilichobaki ni suala la kutambulishwa 

Mbali na nyota hao watatu pia kiungo mwingine ambaye anatajwa kuwa kwenye rada za Simba ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ni pamoja na Nomore Chinyerere ambaye ni kiraka ndani ya kikosi cha FC Platinum ambapo alikuwa anakipiga na kiungo mwenzake Chikwende ambaye yupo zake ndani ya Simba.

Nyota wa tano ni mzawa Abdulmajid Mangalo ambaye yupo zake ndani ya kikosi cha Biashara anatajwa kuhitajika na mabosi hao.

Lengo la maboresho ya kikosi hicho ni kuona kwamba timu hiyo inaweza kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa timu hiyo ni imara na itafanya mambo makubwa katika usajili.

"Kuhusu usajili suala hilo lipo mikononi mwa benchi la ufundi ikiwa kuna wachezaji ambao watakuwa wanahitajika basi tuna amini kwamba tutawapata na tutafanya nao kazi kama benchi la ufundi litakubali,". 

11 COMMENTS:

  1. Stori Lakini ikiwa hivyo Yanga Bingwa,Lakini wasaidie scout maana wenzetu Cha JUU Sana ,mitumba imezidi.Lakini hata hii blog story za kutunga nyingi hasa kwa Simba na Yanga muwe mnatoa matokeo ya Chan .

    ReplyDelete
  2. Lakini ikiwa hivyo Yanga bingwa itakuwa bingwa bia

    ReplyDelete
  3. Yani huyo nimemfuatilia comment zake nyinyi humu mi huwa simuelewi sijui kaanza kushabikia kupitia YouTube eti ka ni hivyo Yanga bingwa Yani kwa sababu Simba inasajili hao wachezaji kwa hiyo Yanga ndo inakuwa bingwa,Kwa wachezaji gani walionao Yanga si ndo walikuwa wanangoza kwa point 8 mpaka Sasa hv zimebaki point ngapi tahira kweli wewe

    ReplyDelete
  4. Kwani idadi ya ukomo wa usajili kwa wachezaji wa kigeni ni ngapi?Mwandishi anasahau kuwa kwa porojo zake ina maana Simba itabidi iachane na nusu nzima ya wachezaji wa kigeni isajili tena hao aliowataja

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba imeruhusiwa na CAF kuongeza wachezaji hadi 10 kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa Africa

      Delete
  5. Ni timu 16 tu bara zima la Africa zinaruhusiwa kusajili wachezaji hadi wakati huu, Yanga labda wasajili line ya simu

    ReplyDelete
  6. nguruwe fc hata msajili mesi na Ronaldo hakuna kitu hapo mavi tu

    ReplyDelete
  7. Manyani FC ukosefu wa kauli ndio zao acheni utopolo wa akili,mavi maana nini?

    ReplyDelete
  8. Kwa akili yako ya kukalili huwezi kunielewa maana ,hata you tube nayo ni mojawapo ya njia ya kutoa taarifa,wewe unayetumia njia sahihi unaona tofauti ya point Kati ya Simba na Yanga ni sawa nadhani una comment kutokea milembe

    ReplyDelete
  9. Nilimwambia mmeingia makundi bt ni round ya pili Napo hukuelewa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. We ndimu hujui chochote kuhusu football Sasa round ya pili waliyocheza na Platinum nayo tutaiitaje,ukibishana sana na chizi we ndo utaonekana chizi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic