UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa kwa sasa unaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kwa timu hiyo kabla ya mechi za Ligi Kuu Bara kurejea.
Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 29 kibindoni.
Imecheza jumla ya mechi 18 huku ikishinda mechi 8,sare 5 na imepoteza jumla ya mechi 5 kwa msimu huu wa 2020/21.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Biashara United, Idrisa Sechombo amesema kuwa mapumziko ambayo waliwapa wachezaji yamekwisha hivyo kwa sasa wameanza maandalizi ya ligi.
"Tuliwapa mapumziko wachezaji wetu ila kwa sasa muda huo tayari umekwisha hivyo tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu za ligi.
"Kila kitu kipo sawa na wachezaji wameanza kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu. Awali tulipanga kucheza mchezo wa kirafiki na Alliance ila mchezo huo umefutwa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment