DILI la kiungo, Doxa Gikanji raia wa Congo limekufa, kwa mujibu wa CEO wa Simba, Barbara Gonzalez.
Barbara amesema kuwa kilichokwamisha dili hilo ni ITC yake ambayo haitoweza kupatikana kwa wakati kwa sababu timu yake ya taifa ya Congo imefuzu hatua ya robo fainali ya CHAN.
Ili kuipata ITC kabla ya dirisha la CAF kufungwa Januari 31 maana yake ni kumwondoa mchezaji huyo kwenye michuano ya CHAN.
Usajili wa Doxa ulizua maswali siku chache zilizopita baada ya jina lake kuonekana kwenye mfumo wa wachezaji waliosajiliwa na Simba kwa ajili ya Ligi kuu Tanzania Bara na ilionekana kuwa raia wa Tanzania (Baadae TFF walitoa taarifa kwamba matatizo kama hayo hutokana na timu nyingi kuingiza majina dakika za mwisho).
Barbara amesema :"Timu ya Congo ipo hatua ya robo fainali Kwenye mihuano ya Chan nchini Cameroon ikiwa tutahitaji ITC yake ina maana kwamba hatakuwa na sifa kushiriki Chan,".
CEO upo vizuri sana kwa kuwa muwazi. Hongera sana kwa kutimiza majukumu yako ipasavyo
ReplyDeleteKuna muda huwa tunakurupuka sana sasa sababu ya kumkata Thaddeo Lwaga kwenye wachezaji wa ligi kuu ni nini?
ReplyDeleteKUNA USHAHIDI GANI KAMA AMEKATWA? ZOTE NI TETESI TU KAMA KAKATWA
ReplyDeleteAhahaha,wanajitekenya na kucheka wenyewe
ReplyDeleteTulikuwa nao wana tosha sana kurejeshs ubingwa na kutufikisha mbali kwengineko. Hongera sana Bibi Barbara nasi tunakukubali kutokana na uwezo wako makubwa na Simba imo mikononi mwa waaminifu shuari kama maji ya mtungi
ReplyDeletegood
ReplyDeleteThey don't have money to sign hime
ReplyDeleteSo strong miss Barbara and we hope harvesting will be high because of your capacity
ReplyDelete