January 29, 2021


 KLABU ya Al Hilal leo Januari 29 imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa Simba Super Cup uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

TP Mazembe anayocheza Mtanzania, Thomas Ulimwengu ilianza kupachika bao kupitia kwa nyota wao Moustapha Kouyate dakika ya 11.

Kwa Al Hilal, dakika ya 29 Bongonga Vinny aliweka mzani sawa na kufanya ngoma kuwa 1-1 baada ya kupachika bao ambalo liliwarudisha wapinzani wao TP Mazembe katikati ya uwanja.

Mpaka wanakwenda mapumziko timu zote mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ndani ya dakika 45, kwenye mashindano ya Simba Super Cup.

Mashabiki ambao walijitokeza Uwanja wa Mkapa walikuwa wachache kiasi chake na walishuhudia ushindani mkubwa ndani ya uwanja.

Kipindi cha pili wachezaji wa Al Hilal waliweza kukosa umakini dakika za mwanzo kupachika bao la pili huku TP Mazembe wenyewe pia wakikosa umakini kupachika bao la pili.

Ikiwa imebaki dakika moja mpira kukamilika, Al Hilal waliweza kupachika bao la pili dakika ya 89 kupitia kwa Mohamed Mussa ambaye alitumia makosa ya mabeki wa TP Mazembe kuokoa hatari iliyokuwa inakwenda langoni kwa kuzamisha mpira kambani.

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Al Hilal ambapo mchezo wa kwanza walipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Simba.

TP Mazembe itamalizana na Simba, Januari 31, Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kilele cha mashindano hayo ambapo msanii wa Bongo Fleva, Zuchu anayemkubali kipa Aishi Manula wa Simba atatumbuiza. 

8 COMMENTS:

  1. Kwa jinsi mambo yalivokwenda na matokeo hayo na hesabu zake, Mnyama ni kifuwa mbele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa picha hii simba bingwa Africa

      Delete
    2. Taarabu fc mmebaki maneno mnyama taratibu anasogea kwenye kilele Cha mafanikio nyie endeleeni kushangilia kuongoza ligi na kombe la mapinduzi.

      Delete
  2. Nyota njema huonekana ahsubuhi

    ReplyDelete
  3. Utopolo visingizio vimekwama kooni.Ohh Al Hilal tinu mbovu.Kafungwa Mazembe kelele za timu mbovu kwisha.Timu mbovu ishiriki makundi ya CAF karibu kila mwaka.
    Acheni ujinga Utopolo.

    ReplyDelete
  4. Dah naiona simba ikiwa nusu fainali klabu bingwa Afrika.big up all leaders board.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic