FAROUK Shikalo, kipa bora kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi leo amerejea rasmi ardhi ya Bongo akitokea nchini Kenya ambako alikuwa amekwenda kwa mapumziko mafupi.
Akiwa ndani ya Yanga kwa msimu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu Bara alikaa langoni kwenye mchezo mmoja kati ya 18 ambayo timu yake imecheza.
Ilikuwa Uwanja wa Mkapa wakati Yanga ikilazimisha kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons na kugawana pointi mojamoja na Prisons ambao hata kwenye mchezo wa pili, Uwanja wa Nelson Mandela ngoma ilikuwa 1-1 ila kipa alikuwa ni Metacha Mnata.
Kwenye Kombe la Mapinduzi alikaa langoni kwenye mechi nne na alifungwa bao moja ndani ya dakika 90 ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Azam FC wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Ilitinga fainali na kusepa na ushindi wa penalti 4-3 mbele ya watani zao wa jadi, Simba baada ya dakika 90 kukamilika kwa wababe hao kutoshana nguvu bila kufungana.
Baada ya ushindi wa Januari 13, wachezaji wa Yanga walio chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze walipewa mapumziko maalumu ambapo leo wanaanza kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment