January 25, 2021

 


MIRAJ Athuman, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa licha ya kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza zama za Sven Vandenbroeck bado anamkumbuka kwa mchango wake ndani ya timu hiyo. 

Miraj hakuwa na bahati na Sven ambapo kwenye jumla ya mechi 15 za Ligi Kuu Bara alicheza mechi tatu huku kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akicheza mchezo mmoja kati ya minne.


Mechi zake za Ligi Kuu Bara ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons wakati Simba ikifungwa bao 1-0, Uwanja wa Sokoine, Simba 2-0 Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru na Mbeya City 0-1 Simba, Uwanja wa Sokoine.


Ule wa kimataifa ilikuwa ni dhidi ya Plateau United ya Nigeria ambapo Simba ilishinda bao 1-0 ugenini.

Sven alibwaga manyanga ndani ya Simba, Januari 7 baada ya kufikisha timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 


Akizungumza na Saleh Jembe, Miraj ambaye wengi hupenda kumuita Sheva amesema:"Kuondoka kwake ni maumivu kwetu kwani alikuwa amejenga mfumo wake ndani ya Simba na tulikuwa tumemzoea ila kwa kuwa ameshaondoka hakuna tunachoweza kukifanya.


"Nilikuwa sipati nafasi kwake ila alikuwa anajua uwezo wangu na kuna vitu alikuwa ananijenga na kunifanya nijiamini zaidi," .

Kwenye Kombe la Mapinduzi, Sheva alicheza jumla ya mechi nne na alisepa na tuzo ya mfungaji bora baada ya kutupia jumla ya mabao manne huko alikuwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola.


Tayari Simba imemtangaza mrithi wa mikoba ya Sven ambaye yupo zake Morocco kuwa ni Didier Gomes Da Rose ambaye tayari amshaanza kazi.

4 COMMENTS:

  1. Maneno yako Miraji ni matamu na ya busara. Mstahamilivu mla mbivu

    ReplyDelete
  2. Ila Simba ilifungwa na Prisons Uwanja wa Mandela Sumbawanga, sio Sokoine!

    ReplyDelete
  3. Madenge sasa mwonyeshe kocha mpya wewe unastahili hamna kisingizio tena

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic