January 25, 2021

 
BAADA ya kumshusha ndani ya Bongo Perfect Chikwende ndani ya kikosi cha Simba akiwa na uhakika wa kushiriki Ligi Kuu Bara leo nyota mwingine wa mabingwa hao watetezi ametua Bongo.

Chikwende tayari ameshaanza mazoezi ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.Wataungana na Kahata mwenye ushkaji mkubwa na Meddie Kagere kusaka ushindi ndani ya Simba.

Imekuwa ikielezwa kuwa Kahata jina lake lipo ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku Chikwende jina lake likiwa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Francis Kahata raia wa Kenya amerejea leo Januari 25 baada ya kupewa mapumziko mafupi na mabosi wake mara baada ya kumaliza kazi ya kusaka Kombe la Mapinduzi ambalo lilikwenda kwa watani zao wa jadi Yanga.

Kahata ambaye msimu wa 2020/21 umekuwa mgumu kwake kutokana na kutokuwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza inaelezwa kuwa mkataba wake ukimeguka anasepa mazima ndani ya kikosi hicho.

Alikuwa amepewa dili la kwenda ndani ya Azam FC kwa mkopo ila aligomea huku mabosi wa Simba wakigoma kuweka wazi hatma ya kiungo huyo mwenye rasta kichwani.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa suala la wachezaji watakaochwa na timu hiyo kwa sasa sio wakati wake kwa kuwa timu inafikiria makubwa ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kahata mwenyewe amesema:"Sijajua hatma yangu ndani ya Simba mpaka pale nitakapozungumza nao kwa kuwa mengi yanasemwa juu yangu.

"Kuna suala la kutolewa kwa mkopo, kuna suala la kuvunjiwa mkataba hilo mimi sijui ninachojua ni kwamba mimi ni mchezaji wa Simba,".

Kwenye  Kombe la Mapinduzi aliweza kuonyesha makeke yake akiwa chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Seleman Matola.

3 COMMENTS:

  1. Anaachwa kwa vigezo gani?Bado no wings bora wa kushoto kwa Simba

    ReplyDelete
  2. Wasituambie swala lakumuacha kahata nyambura simba hatutawaelewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic