January 25, 2021

 


FARID Mussa, kiungo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa kwa sasa hesabu kubwa ni kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Guinea.

Stars ipo kundi D kwenye harakati za kusaka tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali ya Chan inayoshirikisha wachezaji wa ndani nchini Cameroon.

Mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia na iliibuka kifua mbele kwa kuifunga bao 1-0 Namibia kwenye mchezo wa pili.

Ipo nafasi ya tatu na pointi zake tatu ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Guinea ambao ni vinara wakiwa na pointi nne, Januari 27.

Ikiwa itashinda itasonga mbele kwa kuwa itakusanya pointi sita kibindoni na kama itafungwa basi safari ya kurudi Bongo itakuwa imewadia kwa kuwa Zambia imeshafikisha pointi nne na ina faida ya mabao.

Mfungaji pekee wa bao la Stars lililoipa pointi tatu na mchezaji bora kwenye mchezo huo ambaye ni Mussa amesema kuwa wamekubaliana kupambana mbele ya Guinea.

"Mchezo wa kwanza tulipoteza tuliumia ila hatuwezi kubadili matokeo, kwa sasa tunafikiria mchezo wetu ujao dhidi ya Guinea na tunaamini kwamba itakuwa kazi ngumu.

"Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi ili tuweze kusonga mbele kwani kila mmoja anapenda kuona tunapata mafanikio," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic