NYOTA wa kikosi cha Simba, Francis Kahata amesema kuwa yeye bado ni mali ya Simba hivyo taarifa ambazo zinadai kwamba ameondoka ndani ya kikosi hicho yeye hazitambui.
Imekuwa ikielezwa kwamba Kahata ameondoshwa kwa mkopo ndani ya Simba huku wengine wakieleza kwamba amevunjiwa mkataba kwa kuwa nafasi yake kijana Perfect Chikwende ameichukua.
Habari nyingine zimeeleza kwamba Simba wamemuengua Kahata kwenye ushiriki wa Ligi Kuu Bara huku wakimuacha kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa na Chikwende ambaye ni ingizo jipya kuwa kwenye orodha ya wachezaji wa ndani.
Kuhusu hilo Kahata amesema:"Sijui chochote kuhusu kuondoka Simba na kuvunja mkataba ila ninachojua mimi ni mchezaji wa Simba.
"Sijavunja mkataba na wala sijapewa taarifa zozote kuhusu kuondoka ndani ya Simba," .
Kahata ndani ya Simba kabla ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kubwaga manyanga msimu huu wa 2020/21 hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza jambo ambalo limefanya kiwango chake kutokuwa bora.
Anatajwa kuwekwa kando ndani ya Simba ambayo imekuwa na ushindani mkubwa wa namba.
Bado tunamuhitaj kahata! Kijiko nnachokikubali
ReplyDeleteAsepe tu huyo hana lolote!!
ReplyDeleteMimi hapo sitii neno
ReplyDeleteNamuona Kagere naye anajiandaa kufungasha virago vyake
ReplyDelete