IKIWA tayari Klabu ya Simba imeanza maandalizi ya Simba Super Cup baadhi ya wachezaji bado hawajaanza mazoezi na timu kutokana na sababu mbalimbali.
Hawa hapa nane bado hawajaanza kufanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes:-Erasto Nyoni anasumbuliwa na majeraha alikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania ila amerejeshwa Bongo kuendelea na matibabu.
Pascal Wawa alikuwa kwenye mapumziko mafupi pia alikuwa anaumwa wakati anaanza mapumziko wakati ule wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi.
Jonas Mkude ana adhabu yake kutokana na matatizo ya nidhamu.
Joash
Onyango alikuwa kwenye mapumziko.
Aishi Manula yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Cameroon.
Luis
Miquissone alipewa mapumziko.
Said Ndemla yupo kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Cameroon pamoja na Ibrahim Ame.
Kwa hiyo pamoja na kamati ya nidhamu kumuamuru Mkude arejee kambini ndani ya saa 24 bado hajaripoti? John Bocco na Kapombe nao je siyo wapo Cameroon? Mwandishi bhana!!
ReplyDeleteMkude korofii nn??
ReplyDelete