January 26, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao Michael Sarpong anatarajiwa kurejea muda wowote kuanza sasa baada ya kumaliza muda wake wa mapumziko.

Sarpong, wengi wanapenda kuwmita mwili jumba, ametupia mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara alitarajiwa kurejea jana kujiunga na kikosi kambini ila kuna mambo yalikwamisha mpango huo.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Klabu ya Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa nyota huyo atarejea muda wowote kuanza sasa.

"Tayari kikosi kimeanza mazoezi baada ya kuwasili kambini jana, Januari 25 hivyo bado kuna wachezaji ambao wanawasili kambini.

"Kuhusu Sarpong bado ni mchezaji wetu na anatarajiwa kurejea muda wowote kuanza sasa kwa kuwa alikuwa kwenye mapumziko, nchini Ghana," amesema. 

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic