KOCHA mkuu wa klabu ya Biashara
United, Francis Baraza amefunguka kuwa kama kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania, Taifa Stars inataka kusonga mbele katika michuano ya kombe la Mataifa
ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), basi ni lazima
wajitahidi kutumia nafasi wanazotengeneza.
Stars kesho itacheza mchezo wake
wa pili dhidi ya timu ya Taifa ya Namibia mchezo ambao Stars inahitaji kushinda
ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele na kutinga hatua ya robo fainali,
hii ni baada ya kupoteza kwenye mchezo wa kwanza mbele ya Zambia.
Baraza amekuwa na msimu mzuri
kwenye ligi akiiongoza Biashara kukamatia nafasi ya nne kwenye msimamo na
pointi zao 29 walizokusanya kwenye michezo 18.
Akizungumzia nafasi ya Stars
Baraza amesema: "Bado naamini Stars ina nafasi ya kufuzu hatua inayofuata
hii ni kama tutaweza kuwa na matumizi mazuri ya nafasi tunazotengeneza, vijana
wetu wanapaswa kujituma zaidi,"
Duh maoni yako tumepokea, kesho ni draw ngoma
ReplyDelete