January 31, 2021

 


MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga,  Fiston Abdulazack tayari ameanza mazoezi ndani ya kikosi cha Yanga kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho. 


Nyota huyo ametua ardhi ya Bongo  Januari 29 na kujiunga na timu hiyo ambayo inanolewa na Kocha Mkuu,  Cedric Kaze.


Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 kwa msimu wa 2020/21.


Mratibu wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zao zijazo na wanaamini wataendelea kufanya vizuri.


"Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo na tunaamini kwamba tutafanya vizuri kwa kuwa kila mmoja anaonelana kupenda kile anachokifanya.


"Wachezaji wameanza mazoezi tangu Januari 25 hata mchezaji wetu Fiston naye ameanza mazoezi, " .

2 COMMENTS:

  1. Mungu ni mwema tutapamba hadi mwisho.Daima mbele nyuma mwiko

    ReplyDelete
  2. Usajili wa beki Job kutoka Mtibwa na Fiston raia wa Burundi umekuwa ni usajili wa Kimkakati na Utakuwa na Tija sana. Bravo Young African Sports Club

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic