VIVIER Bahati, kocha msaidizi wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa bado vijana wake wanazidi kuimarika jambo ambalo limewafanya waibuke na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC.
Azam FC iliibuka na ushindi huo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Januari 29, Uwanja wa Azam Complex.
Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na Prince Dube na moja lilipachikwa na Mudhathir Yahya huku lile la KMC likipachikwa na Lusajo Mwaikenda aliyepachika bao hilo kwa penalti.
Bahati amesema:"Ulikuwa ni mchezo mzuri na kila mchezaji alikuwa kwenye wakati mzuri jambo ambalo limetufanya tuwe katika wakati mzuri kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinakuja,".
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kurejea Februari 13 huku Azam FC ikiwa na kibarua cha kuanza kumaliza kiporo cha mchezo wake dhidi ya Simba.
Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Februari 7, Uwanja wa Mkapa.
Mtaje na vkosi vlivocheza bac,,,co kutupa magoli na wafungaji tu
ReplyDelete