KOCHA Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa uwezo wa nyota wake John Stones unazidi kuimarika kila leo jambo linalomfanya ajivunie uwepo wake.
Usiku wa kuamkia leo, City ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Crystal Palace, Chelsea wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Etihad.
Kwenye mchezo huo Stones alifunga mabao mawili dakika ya 26 na 68 na Likay Gundogan alitupia moja dakika ya 56 na lile la mwisho lilipachikwa na Raheem Sterling dakika ya 88.
Ushindi huo unaifanya City kuishusha Liverpool ambayo ililazimisha sare ya bila kufungana na Manchester United iliyo nafasi ya kwanza na pointi 37, City inafikisha jumla ya pointi 35 huku Liverpool iliyobanwa Anfield ikiwa nafasi ya nne na pointi 34.
Pep amesema:"Ni furaha kuona kwamba timu inapata ushindi ndani ya uwanja, Stones amekuwa akifanya vizuri ndani ya uwanja jambo ambalo linaleta furaha, bado kuna kazi ya kufanya kwa ajili ya mechi zetu zijazo,".
0 COMMENTS:
Post a Comment