KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Zambia, Sredojevic Milutin Micho amekiri kwamba anatarajia kukutana na mchezo mgumu dhidi ya Taifa Stars leo.
Zambia leo itacheza dhidi ya Taifa Stars kwenye mchezo wao wa
kwanza wa kundi D la michuano ya CHAN, mchezo utakaopigwa jijini Limbe, Cameroon
majira ya saa 1:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Akizungumzia mchezo huo Micho amesema: “Tunaiheshimu Tanzania
kwakuwa najua wana ligi ya ndani nzuri na imara, najua ubora wao mpaka kufikia
hapa ila tumejiandaa kupambana nao leo hii,”
Hizi ni fainali za tatu kwa Micho ambaye amewahi kupita
kwenye kikosi cha klabu ya Yanga, ambapo fainali mbili za kwanza alikuwa
akikiongoza kikosi cha Uganda mwaka 2014 na 2016.
Zambia piga hao wababaishaji bao 5-0
ReplyDeleteWewe ni mkichaa
DeleteKweli kabisa wababaishaji, tumepigwa 2:0
ReplyDelete