MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Simba raia wa Nigeria, Junior
Lokosa amefunguka kuwa malengo yake makubwa ya kujiunga na Simba ni kuja
kushinda mataji kwenye michuano yote iwe ya ndani au ile ya kimataifa.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na kutambulishwa rasmi kuwa
mchezaji wa Simba siku ya Jumatatu amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya
kuachana na klabu ya Esperance ya Tunisia aliyoitumikia msimu uliopita.
Ukiachana na Esperance, Lokosa pia amewahi kukipiga na klabu
za Kano Pillars na First Bank za kwao Nigeria.
Akizungumzia malengo yake baada ya kusajiliwa na Simba Lokosa
alisema: “Nafurahi kukamilisha usajili wangu ndani ya kikosi cha klabu ya
Simba, hii ni heshima kubwa kwangu kwa kuwa Simba ni timu kubwa Afrika.
“Kuhusiana na
matarajio nisingependa kusema mengi lakini naahidi kujituma kwa uwezo wangu
wote kuhakikisha naisaidia Simba kuwa mabingwa wa Afrika kwa kushinda taji la
Ligi ya mabingwa Afrika, lakini pia kushinda taji la Ligi Kuu ya Tanzania.
“Najua mashabiki wa
Simba wanatarajia mambo mengi kutoka kwangu, naamini taratibu nitaweza
kuwafurahisha kwa kuionyesha kiwango cha juu,”
0 COMMENTS:
Post a Comment