KLABU ya soka ya Yanga, tayari imemtangaza, Edem Mortotis kuwa kocha wao mpya wa viungo na utimamu wa mwili ambaye anakuja kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na raia wa Afrika Kusini, Riedoh Berdien aliyeondoka mwishoni mwa msimu uliopita.
Mortotis alitua nchini siku ya Jumanne na kupokelewa na mwenyeji wake Injinia. Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa klabu ya Yanga na mjumbe wa kamati ya usajili na kwenda kusaini mkataba tayari kwa ajili ya kuanza majukumu yake mapya.
Yanga ipo kwenye mipango ya
kuimarisha benchi lake la ufundi kwa ajili ya kuwa na kikosi imara ambacho
kitafanikisha lengo lao la kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kombe la FA.
Hii hapa sehemu ya wasifu wa kocha huyo;
Ni mzaliwa wa jiji la Accra Ghana, ambaye amewahi kusoma nchini Canada ambapo alikuwa akiendeleza kipaji chake cha soka na timu ya KC Trojan.
Baada ya hapo akaenda kusoma chuo cha Northern Alberta Institute of Technology cha hapo hapo Canada wakati huo anaendelea kutunza kipaji chake kupitia timu za chuo hicho.
Alipomaliza masomo yake Edem akapata nafasi ya kuitumikia timu ya akiba ya Fc Edmonton, akadumu hapo hadi 2013 alipopandishwa na kupewa mkataba na timu ya wakubwa.
Mwaka 2017 akapelekwa Edmonton
Victoria akafanikiwa kucheza mechi 10 na kuifungia mabao 2, Msimu wa 2017
ulivyomalizika akajiunga na Edmonton Green & Gold akacheza mechi moja na
kufunga bao moja, msimu uliofuatia wa 2018 akacheza mechi tano tu, Januari 2019
akarejea Fc Edmonton, hapo akacheza mechi 18 za Ligi baadae Novemba 2019
wakampa mkataba mpya tayari kwa msimu wa 2020
Jamani mbona tunaleta utani kwenye mpira wetu wa miguu hapa tz yaani cv haieleweki kamisa yaaninka kabisa hakuna cv hapo ni ubabaishaji huo timu kubwa inaleta kocha mkubwa wa viungo ila huyu siyo kabisa atamaliza hela zetu hapa .....nina imani pale Udsm wapo walimu wazuri wa viungo kuliko huyu hapa acheni uvivu wananchi.
ReplyDelete.
Hela unatoa wewe? Wewe ndie ulieagiza aletwe? kama inakukera hamia Simba, hujalazimishwa kushabikia Yanga.
DeleteUmeona EEE
DeleteMbona cv nyepesi sana?
ReplyDeleteToa CV yako iliyo NZITO kama hiyo unaona nyepesi.
DeleteMbona CV yake ni ya kucheza mpira kuliko ukocha uliomfanya apate ajira yanga... Watu washapiga cha juu hapo
ReplyDeleteUnawezaje kuwa kocha bila kuujua mpira na ukajua na kuucheza? hoja yako haina mashiko kama wewe unajiona kocha kaombe ajira Yanga.
DeleteUkocha co lazima uwe umecheza mpira.. wapo makocha wengi tu wazur na hawajacheza mpira.... Ishu hapa ni kwamba unapoajir kocha bac cv yake inabidi ibez kwenye ukocha... sasa kinachoonekana hapo ni sawa na kuajiri daktri wa meno halafu cv yake inaelezea udaktari wa mifupa.... Daah natumia nguvu nyingi kumuelewesha UTOPOLO
DeleteHUYO SIO KOCHA WA FITNESS WALA TUSIDANGANYANE, NI MCHEZAJI. VYOMBO VYA HABARI NA TOVUTI KUBWA VINARIPOTI KWAMBA YANGA WAMESAJILI KIUNGO....DUNIA HAIJUI KAMA HUYU NI KOCHA WA FITNESS. LESENI YAKE IPO WAPI? KAMA WEWE BINGWA WA KUBISHA INGIA MTANDAONI ANDIKA JINA LAKE UTAONA UTAKACHOLETEWA
DeleteHii ni kali sana. Muandishi anamsifu Kocha mpya wa Yanga wa viungo kwakuwa katika mechi kumi alizocheza, alitia magoli mawili
ReplyDeleteKama ulimsikia vizuri engeneer ni kwamba ame tlain maswala ya fitness,but nachotaka kuamini mm ni kwamba huyu jamaa,msimu ujao ni mchezaji wa yanga,may not it
ReplyDeleteSasa mbona mnatuchanganya, kasajiliwa kama mchezaji au kocha? Au player cum coach? Ila kiukweli hana cv ya ukocha wowote labda tunafichwa. Au tumesajili mganga wa jadi toka Ghana? Natania tuu tusiporomoshe mitusi bure
ReplyDeleteUtopolo kila kitu
ReplyDeleteUsiwaze hata kidogo jombaaa wewe noa visu vyetu lengo tujaze makombe
ReplyDeleteCv yake inaleta maswali mengi. Naamini watu wa wizara ya kazi watatenda haki Tanzania kuna watu wengi wana qualifications zaidi ya huyo. Kutakuwa na shida kupata work permit
ReplyDeleteDah Kwa vigezo gani huyu kocha anapewa 'work permit'ya kufanya kazi as a 'physical training coach'kwa CV yake uliyoimwaga hapa?Au Eng.Hersi mlipata Musoma wote huko Canada...Acheni masihara na ajira Kwa watanzania...hii ni dharau Kwa wanazuoni wa professional hii.Pengine ni ushauri wa Tiboroha.
ReplyDeleteJaman hebu tufikie sehem tige upande wa pili Kama tunataka kufanikiwa
ReplyDeleteHii kari sana utopolo kwahili mmechemsha
ReplyDeleteNahisi utopolo huyu mmeingizwa chaka
ReplyDeleteHuyo ni mchezaji ambae amekuja kuongeza ufundi wa middle zetu ila mwakani yuko uwanjani mwenyewe kwahyo tumia akili kufikili Yanga inatumia akili nyingi so subr yajayo yanafurahisha.
ReplyDelete