NYOTA wa kikosi cha Simba, Bernard Morrison
ameweza kuweka rekodi tatu za ajabu ndani ya Uwanja wa Mkapa kama namba yake ya
jezi inavyosoma mgongoni.
Nyota
huyo anaweka rekodi ya kwanza kuwa nyota wa kwanza kufunga mabao mawili ndani
ya dakika tatu na kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano pamoja na
ile staili ya kushangilia huku mpira ukiwa ndani ya bukta.
Morrison
ameweka rekodi yake ya kufunga mabao mawili ndani ya dakika tatu ilikuwa Uwanja
wa Mkapa kwenye mchezo wa Simba Super Cup, Januari 27 ambapo alifunga bao la
kwanza dakika ya 86 ambapo alishangilia kwa kuweka mpira ndani ya bukta na lile
la pili alifunga dakika ya 89.
Pia
ndani ya dakika 27 ambazo alitumia Morrison akitokea benchi kwa kuchukua nafasi
ya Francis Kahata aliweza kuwa mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano
dakika ya 90+3.
Morrison amesema:”Ninafurahi kufunga na ninapenda kuwa na furaha ndani ya Simba, nina amini mashabiki wanapenda kuona tunafanya vizuri hivyo tutazidi kupambana,”.
Leo Simba ina kazi ya
kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa pili ambao ni wa kilele cha
Simba Super Cup dhidi ya TP Mazembe.
0 COMMENTS:
Post a Comment