UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa maendeleo ya nyota wao watatu ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ambao ni Saido Ntibanzokiza, Yacouba Songne na Dickson Job yanaleta matumaini hivyo mashabiki wasiwe na presha.
Saido ambaye ni kiungo mshambuliaji aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons huku Yacouba alipata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi hatua ya robo fainali dhidi ya Azam FC na Job yeye alipata maumivu ya paja akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi huku wale wanaosumbuliwa na majeraha wakiwa na maendeleo mazuri.
“Kuhusu Job huyu tayari ameanza mazoezi mepesi na wachezaji wenzake ambao wapo kambini hivyo tupo imara na nina amini kwamba mpaka ligi itakaporudi kila kitu kitakuwa sawa.
“Yacouba na Saido nao pia bado hawajawa fiti ila nao maendeleo yao ni mazuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu wachezaji hawa,” alisema Saleh.
0 COMMENTS:
Post a Comment