January 24, 2021


 IKIWA leo Januari 24 mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wamemtambulisha mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba ameanza kazi rasmi.

Mrithi wa Sven ni Didier Gomes Da Rosa ambaye ametua Bongo leo na kusaini dili la miaka miwili ametambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari na Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez akiwa sambamba na mpiga mgenga, Haji Manara ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Habari.

 Didier Gomes Da Rosa ambaye ni raia wa Ufaransa amekanyaga kwa mara ya kwanza Uwanja wa mazoezi wa Klabu ya Simba wa Mo Simba Arena.

Anaanza kukinoa kikosi hicho ambacho kimetinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na mchora ramani alikuwa ni Sven ambaye kwa sasa yupo zake ndani ya kikosi cha FAR Rabat ya Morroco.

Atafanya kazi kwa ushirikiano na mzawa, Seleman Matola ambaye kwa sasa yupo na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyopo nchini Cameroon kwa ajili ya kushiriki michuano ya Chan.

9 COMMENTS:

  1. Didier Gomez kabla ya Almerekh ya Sudan alifanya kazi Egypt Ismailia pia.Inashangaza lakini yamekuwa kwani Alhaly waliihofu Almerekh ya Sudan kwa sababu ya uwepo wa Gomez ndani ya kikosi hicho cha Sudan.Hii mikakati ya simba kuelekea hatua ya makundi ni hatari.Inatetemesha Ukisikia Alhaly wamebadolisha kocha usishangae. Wachezaji wa kimkakati,makocha wa kimkakati inaonehsa kiasi gani simba walivyosiriaz kuiekea heshima Bendera ya nchi.Ligi yetu imeongezeka samani.kuna mambo mengi yamechangia ligi yetu kuonekana ila kama watanzania tisiwe wanafiki na tusione aibu kusema kuwa simba ni miongoni mwa muakilishi anaeiwakilisha nchi yetu vyema kimataifa kiasi cha kuipa ubora ligi yetu pia.kongole Mo,kongole Barbara.Dada yetu huyu ni wa next level kusema kweli.Mambo haya makubwa yanayotokea simba yanahitaji viongozi jasiri sana chini ya mtendaji mkuu mahiri na ni vyema wanasimba na watanzania wenye nia njema kuunga mkono jitihada za simba kwenye klabu bingwa Africa kwa manufaa ya taifa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. WeWe Ni mwanamichezo umeandika vizuri sana simba imeipa thamani kubwa ligi yetu kama wameweza kumchomoa kocha kutoka almereikh hakika mikakati yao inastahili pongezi wapo serious kweli na mashindano hayo kongole kwao

      Delete
  2. Simba's alarming roar with God's will, will be heard across Africa

    ReplyDelete
  3. Yes, God is Great And Willing

    ReplyDelete
  4. Kwakuwa Simba wanayo Simba Day nasi pia tulifanya yetu ili tusionekane wanyonge na kwakuwa sasa wameleta mpya Super Cup nasi tupo mbioni kutafuta kingine na hayutski Kusikia eti tunaiga HAHAHAAA

    ReplyDelete
  5. Yetu macho... corona haiwezi kuokoa jahazi kila wakati

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic