KIUNGO wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ amepata majanga akiwa na kikosi cha timu hiyo visiwani Zanzibar ambapo amerudishwa jijini Dar na kuikosa michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani humo.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kikosi kipo vizuri, wachezaji wote wapo fiti isipokuwa Carlinhos ambaye amerejeshwa Dar.“
Anatakiwa kuendelea na matibabu pamoja na program alizokuwa amepangiwa kutokana na kutokuwa fiti.”
Kikosi cha Yanga jana kilifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC.
Mchezo wa kwanza Yanga ililazimisha sare ya bila kfungana na Klabu ya Jamhuri ambapo nyota huyoo raia wa Angola hakuwepo benchi.
Niliwahi kucoment humu mwanzoni kabisa alipokuja nchini nilisema huyu jamaa anaonekana hayupo fit. Alikuwa anapiga mipira ya kona haifiki golini kwa adui. Watu walinisema sana.
ReplyDeleteMipira ya kona haifiki golini?
DeleteLamine alikuwa anafungaje kama haifiki?
kama hakua fit mlimpeleka zanzibar kufanya nn yaani viongozi yanga mnaakili za kuvukia barabara tu
ReplyDeleteMchezaji ana kilo 40 atachezaje mpira?Tulisajili fotomodel tena kwa maandamano. Huyu Hersi hakujua historia ta mchezaji huyo?Au sifa tu!!!
ReplyDelete