January 19, 2021


 MATUMAINI ya mtambo wa mabao ndani ya Yanga, Carlos Carlinhos raia wa Angola kurejea ndani ya uwanja kwa sasa ni hafifu kwa kuwa bado yupo kwenye matibabu.

Nyota huyo alitonesha maumivu yake ya nyonga ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati wakishinda mabao 2-1.

Alipanda boti mpaka visiwani Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Mapinduzi ila alirejeshwa fasta Dar ili kuendelea na matibabu baada ya kujitonesha mazoezini.

Yanga ikiwa imefunga mabao 29, Muangola huyo amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao manne.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa bado anaendelea na matibabu ya nyonga hivyo akiwa fiti itajulikana muda wake wa kurejea uwanjani.

"Bado kwa sasa Carlinhos anaendelea na matibabu hivyo akipona itafahamika anaweza kurejea lini uwanjani ndani ya uwanja," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Sema tuu yanga wanafanya uungwana, huyu bwana hakuwa fit tangu alikotoka. Nilisema mapema sana kuwa huyu anaonekana hawezi vurugu za ligi kuu maana alikuwa legelege mno. Tumeombee apone

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wangekuwa waungwana wangelipa bila shida madeni yote wanayodaiwa na baadhi ya waliowahi kuwa wachezaji wao

      Delete
    2. Usiwe mjinga wa mawazo jua kuwa uungwana sio kwamba usdaiwe. Hata
      nchi inadaiwa sembuse Yanga

      Delete
  2. Mungu atamsaididia tu na atarejea katika ubora wake kwani Carlos ni mchezaji mzuri sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic