January 23, 2021

 


JUNIOR Lukosa raia wa Nigeria leo Januari 23 amewasili Bongo kumalizana na Simba kwa ajili ya kutumika ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo utambulisho wake unatarajiwa kufanyika kwenye mashindano ya Simba Super Cup.


Nyota huyo ana umri wa miaka 27 aliletwa duniani Agosti 23,1993 huko Badagry,Nigeria ndiko ambapo alizaliwa.

Rekodi zinaonyesha kuwa mshambuliaji huyo wa kati alikuwa ndani ya Klabu ya Kano Pillars msimu wa 2018-19 alicheza jumla ya mechi 35 na kutupia jumla ya mabao 23.

Msimu wa 2019-20 alikuwa ndani ya Klabu ya ES Tunis ambapo alicheza mechi 11 na kutupia mabao mawili na kwenye timu ya Taifa ya Nigeria amecheza mchezo mmoja pekee mwaka 2018.

Anakuja kuchukua nafasi ya Charlse Ilanfya ambaye alifeli kuonyesha makeke yake ndani ya Simba na kwa sasa yupo zake kwa mkopo ndani ya Klabu ya KMC.

1 COMMENTS:

  1. Ilanfya hajafeli kuonyesha kiwango,, n kwamba hajaaminiwa na sven. Jamaa yuko vzr sema damu yake na ya sven zilkuwa hazipendani. Ht miraji alisota mno benchi lakn cheki kiwango alichokionyesha kule zanzibar,! Makocha wa timu
    kubwa za bongo simba na yanga huwa wanaua sn viwango vya wachezaji wetu kwakweli.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic