IMEBAINIKA kuwa
sababu iliyomuondoa aliyekuwa kocha msaidizi wa kikosi cha klabu ya Yanga, Juma
Mwambusi ni matatizo ya jino.
Mwambusi alitangaza uamuzi huo Januari 21, mwaka huu ambapo
aliwasilisha barua kwa uongozi akiomba kupumzika na kutumia muda huo kwa ajili
ya matibabu.
Mwambusi alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akiwa
kama kocha msaidizi wa Mserbia, Zlatko Krimpotic ambaye baadaye alifutwa kazi na
nafasi yake kuchukuliwa na Mrundi Cedric Kaze.
Akiwa na kikosi cha Yanga mwambusi alihudumu kama kocha
msaidizi kwenye michezo 18 ya ligi na kufanikiwa kushinda michezo 13 huku wakitoa
sare michezo mitano.
Akizungumzia kuhusu afya yake Mwambusi alisema: “Ushauri wa Daktari ndiyo umesema
nipumzike, wiki inayokuja ndiyo nitaenda kufanyiwa upasuaji Muhimbili ili
kuondoa jino zima lakini kwa sasa nimeanza matibabu madogo madogo, naomba
Watanzania waniombee,”
Bdio mnataka tuamini hilo? Mmenoa, semeni ukweli kaze analeta mtu wake
ReplyDeleteKwan hata Kaze akileta mtu wake inakuhusu nini ndugu?
DeleteYaleyale!!,pilipili ucyoila...?
ReplyDeleteYaleyale!!,pilipili ucyoila...?
ReplyDeleteUTOPOLO wameshazoea kudanganywa .... kuumwa jino ndo aache kazi?
ReplyDeleteUtopolo bwana jino jamanidu aibu tutaelewana tu
ReplyDelete