JUNIOR Lokosa mwili jumba, mshambuliaji wa zamani wa Klabu ya Esperance raia wa Nigeria amemalizana na Simba na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki na kufanya timu hiyo iwe na washambuliaji asilia wanne.
Mshambuliaji wao namba nne ambaye alikuwa ni chaguo la Sven Vandenbroeck kwa mujibu wa Simba Charlse Ilanfya amepelekwa kwa mkopo alikotolewa ndani ya KMC.
Mshambuliaji huyo ambaye aitua kwenye ardhi ya Bongo Januari 23 kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Simba ambao ni mabingwa watetezi amesaini dili la miezi sita.
Nyota huyo ana umri wa miaka 27 aliletwa duniani Agosti 23,1993 aliweza pia kutumika ndani ya Kano Pillars msimu wa 2018-19 alicheza jumla ya mechi 35 na kutupia jumla ya mabao 23.
Atatambulishwa rasmi kwa mashabiki Januari 27 kwenye mashindano ya Simba Super Cup ambayo yanayoshirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyewe wakiwa ni wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe.
Safu ya ushambuliaji ya Simba itakuwa inaongozwa na nahodha John Bocco, Meddie Kagere, Chris Mugalu na Junior.
Welcome Lokosa! Upge kazi haswa lakn coz tuna matumaini makubwa sn toka kwako!
ReplyDeleteNa hapo ndipo atapojulikana Mnyama. Nyoyo zimejaa hofu zimewajaa na mbwembwe siku hizi haisikiki tena
ReplyDeleteSIMBA BABA LAO
ReplyDelete