MICHAEL Sarpong mshambuliaji ndani ya kikosi cha Yanga alipata nafasi ya kutoa msaada kwenye kituo cha Royal Seed Orphanage kilichopo nchini Ghana wiki hii.
Sarpong alirejea Ghana, Januari 13 baada ya kumaliza kazi ya kusaka Kombe la Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Ndani ya Ligi Kuu Bara ametupia mabao manne wakati timu yake ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo na anatarajiwa kurejea leo kujiunga na kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.
Pia nyota mwingine ambaye alifanya kama Sarpong kwa kurejesha kwa jamii ni Mukoko Tonombe ambaye yeye jana Januari 24 alitembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni, Mkwajuni.
This is Professionalism
ReplyDeleteGhana kuna azam cola? Kweli huu ni ushamba
ReplyDelete