UONGOZI wa Yanga umesema kuwa baada ya kumaliza kazi ya kutwaa taji la Kombe la Mapinduzi nguvu inahamia ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedrick Kaze inafikisha jumla ya mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi kabatini huku mtani wake Simba akiwa na mataji matatu kibindoni.
Kikosi hicho kilitwaa ubingwa huo kwa kuiadhibu Simba kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya bila kufungana.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa kazi ni kubwa kwa sasa wanaiwekeza kwenye ligi.
"Tumetwaa taji la Mapinduzi hii ni furaha kubwa kwetu, kazi ya kwanza imekwisha sasa nguvu zetu inahamia kwenye Ligi Kuu Bara, hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti," amesema.
Sawa
ReplyDeleteLigi kuu hamchukui ng'oo, wala msijidanganye
ReplyDeleteKwasababu unacheza wewe hawawez kuchukua
ReplyDeleteMwaka huu hamubebwi.mulishazoea kubebwa mtabeba mno nyau mpaka wegine watazalia uwajan.mnaenda nanyau kunapanya humo uwanjan?waachen majumban wafukuze panya majumban kwenu
ReplyDeleteHao upande was pili wengi maimuna , huwezi amini mpaka Leo wanatamba wameingia makundi Lkn hawajui Kama ni round ya pili ukiwambia wanabishi wanakuita nyani eti nadhani laana ya mafisango bado inawatafuna mbumbu hao
ReplyDelete