January 16, 2021


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa ndani ya mzunguko wa pili watapambana kufanya vizuri ili kurejea kwenye ubora ndani ya uwanja.

Kikosi hicho kilicho chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye amechukua mikoba ya Zuber Katwila ambaye yupo zake ndani ya Ihefu FC hakijawa na mwendo mzuri ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kikiwa kimecheza jumla ya mechi 18 kimekusanya jumla ya pointi 22 kikiwa nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kinara ni Yanga ana pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na walipokutana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kikosi cha Yanga kilishinda bao 1-0 na kusepa na pointi tatu mazima.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa watapambana ndani ya uwanja ili kupata matokeo mazuri.

"Tumekuwa kwenye mwendo mbaya hili lipo wazi ila kwa wakati ujao wa mzunguko wa pili tutakuwa imara na tunaamini kwamba tutapata matokeo mazuri.

"Mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani tunaamini kwamba wanahitaji kupata matokeo mazuri nasi pia tutafanya vizuri," amesema.

Mhimili wao namba moja kwa upande wa mabeki, Dickson Job yupo zake ndani ya kikosi cha Yanga akiwa amesaini dili la miaka miwili. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic