February 26, 2021


 NYOTA wa timu ya JKT Tanzania, Adam Adam ambaye kwa sasa yupo zake nchini Uturuki amesema kuwa mawazo yake ni kucheza nje ya nchi jambo ambalo analiomba liweze kutimia.

Adam ametupia mabao 7 ndani ya Ligi Kuu Bara ni kinara wa utupiaji ndani ya JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed.

Yupo huko kwa ajili ya majaribio ya muda wa wiki moja ili aweze kupata nafasi ya kupata dili la moja kwa moja huko.

Akizungumza na Saleh Jembe, Adam amesema kuwa anaamini kwamba mambo yatakuwa sawa kwake katika kutimiza ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa nje ya Bongo.

"Ninafikiria kuhusu kucheza nje kwa sasa na sio ndani ya Bongo kwa kuwa nahitaji kupata changamoto mpya.

"Maombi yangu ni kuona kwamba hili nalo linafanikiwa kwa kwa ni ndoto yangu ya muda mrefu na nina amini itakuwa sawa," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic