KINDA Jahkeele Marshall-Rutty anatajwa kuziingiza vitani klabu kubwa duniani ambazo zinahitaji saini yake ikiwa ni pamoja na Chelsea, Manchester United, Manchester City ambazo zinapata ushindani pia kutoka Bayern Munich na Juventus.
Nyota huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Toronto mkononi ana tuzo ya kuwa mchezaji bora ndani ya timu hiyo ambayo aliitwaa Oktoba,2020 yeye ni mshambuliaji na ana miaka 16.
Aliletwa duniani Juni 2004 amekuwa akitajwa kuwa ni bora awapo ndani ya uwanja jambo ambalo limezifanya timu nyigi duniani kubwa kumfuatilia kwa ukaribu ili kuwa naye katika timu zao kwa ajili ya wakati ujao.
Imeripotiwa kuwa Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola anahitaji kuwa naye ndani ya kikosi chake kwa kuwa anakubali uwezo wake jambo ambalo litampa changamoto ni ushindani kutoka timu nyingine ambazo zinahitaji saini yake.
Kinda huyo raia wa Canada amesema kuwa anachotazama kwa sasa ni kuona anafika hatua ya mafanikio ambayo anayatarajia bila kujali amevunja rekodi ya nani ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment