February 27, 2021


 MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa timu ya Arsenal amesema kuwa anaamini kwamba mshambuliaji wake Pierre Aubameyang atafunga mabao mengi.

Msimu huu wa 2020/21, Aubameyang amekuwa akiandamwa na ukame wa mabao jambo ambalo linampa wakati mgumu raia huyo wa Gabon.

Arteta amesema kuwa anaamini mapito ambayo anayapitia nyota huyo yatapita na kurejea kwenye ubora wake.

"Bado yupo vizuri na anaweza kufanya mambo mengi ndani ya uwanja hivyo wakati unakuja ambapo ataweza kufunga na kutupa matokeo mazuri.

"Namuamini kwa kuwa amekuwa akitengeneza nafasi na anatumia nafasi ndani ya uwanja hivyo bado ana muda wa kurejea ndani ya uwanja hivyo sina mashaka naye," .  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic