BAADA ya kuonyesha kiwango bora akicheza mechi yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, kiungo mshambuliaji wa Simba, Perfect Chikwende amefunguka kuwa mashabiki watarajie makubwa kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Jumapili.
Chikwende aliingia dakika ya 61 akichukua nafasi ya Luis Miquissone ambapo alifanikiwa kutoa pasi ya bao kwa Bernard Morrison aliyefunga dakika ya 66 na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC kwenye mchezo uliopigwa juzi Alhamisi kwenye Dimba la Jamhuri jijini Dodoma.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Chikwende ambaye alitakiwa na Azam FC kwenye dirisha dogo kabla ya kujiunga na Simba alisema: “Namshukuru Mungu nimeweza kuchangia ushindi wa timu yangu na kuipa pointi tatu muhimu, kwa sasa najikita kwenye mechi dhidi ya Azam FC, mashabiki wetu watarajie makubwa kwani malengo yetu ni kufanya vizuri kwenye kila mchezo ambao tutashuka dimbani.
”Simba imefikisha pointi 38 baada ya kushuka dimbani kwenye mechi 16 ikishinda mechi 12, sare mbili na imepoteza mechi mbili ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara nyuma ya vinara Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment