February 27, 2021


 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ndani ya ardhi ya Tanzania, Simba wamerejesha tabasamu lao upya baada ya majembe yao matatu ya kazi kurejea rasmi kweye kikosi hicho.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, jana Februari 26 ubao ulisoma African Lyon 0-3 Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora na kuwafanya waweze kutinga hatua ya 16 bora.

Kwenye mchezo huo majembe mawili ambayo yalikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali yalianza rasmi kwenye kikosi kazi. John Bocco ambaye alikuwa ni majeruhi na Jonas Mkude ambaye alisimamishwa kutokana na nidhamu.

Hawa wote walicheza ambapo Mkude, kiungo mkabaji yeye aliyeyusha dakika zote 90 huku Bocco akitokea benchi kipindi cha pili na kucheza kwa mara kwanza mbele ya Gomes.

Leo Februari, Patrik Rweyemamu ambaye alisimamishwa na mabosi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa ni hujuma baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo amerejeshwa kikosini.



Rweyemamu alisimamishwa na Simba na nafasi yake ambayo alikuwa ni meneja ilikuwa mikononi mwa Abas Seleman ambaye kwa sasa atarejea nafasi yake ya kuwa mratibu.

Kikosi cha Simba kwa sasa kinajiaandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ubao ulisoma JKT Tanzania 0-4 Simba.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic