February 28, 2021



KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amefunguka kuwa, licha ya kikosi cha timu hiyo kushiriki mashindano mengi tofauti, lakini hawajasahau michezo yao mitatu ya viporo kwenye Ligi Kuu Bara ambayo wanataka kushinda ili kupanda mpaka kileleni mwa msimamo.

Simba inakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imekusanya pointi 42 baada ya kucheza mechi 18, ikizidiwa kwa pointi saba pekee na vinara wa msimamo klabu ya Yanga ambayo imekusanya pointi 49 katika michezo yao 21 waliyocheza mpaka sasa.

Kesho Jumatatu, Simba inatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na JKT Tanzania katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu, utakaopigwa katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mipango yao, Gomes amesema: “Hivi karibuni ratiba yetu imetubana kidogo kwani tumekuwa na michezo mingi ya michuano tofauti, lakini ni jambo zuri kuona tunapata matokeo mazuri kwenye michezo yote.

“Licha ya michuano mingi tuliyonayo, lakini nikuhakikishie bado tunakumbuka kuwa tuna michezo mitatu ya ligi ambayo lazima tushinde, kwani tunataka kushika usukani wa ligi katika kipindi hiki ambapo ligi inaelekea ukingoni ili kujihakikishia malengo yetu ya kutwaa ubngwa msimu huu,”


2 COMMENTS:

  1. Kila la kheri MNYAMA kwenye mashindano yote unayoshiriki.... Kwa sasa mpira unaopiga mkubwa Sana,tunakuaminia

    ReplyDelete
    Replies
    1. We, uto wanalosikia hivo, loh! Wanna Wanajua yanayowasibu mioyoni😋😋

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic